Habari

Aliyeoa wake 24 na kujaliwa watoto 145 afungwa jela

Wanaume wawili ambao ni viongozi wa kidini nchini Canada wametiwa hatiana na mahakama nchini humo kwa kosa la kuoa wake wengi. Winston Blackmore mwenye umri wa miak 61 alioa wanawake 24 na inakadiriwa amejaliwa kupata watoto 145 , na mkwe wake James Oler akaoa wanawake watano.

Winston Blackmore na familia yake

Baada ya kupatikana na hatia kila mmoja anakabiliwa na kifungo cha miaka mitano jela, hata hivyo hukumu hiyo imetajwa kuwa mtihani mkubwa kwa uhuru wa kidini nchini humo.

Blackmore na Oler wote walikuwa ni makasisi wa dhehebu lililojitenga kutoka kanisa la Fundamentalist Church of Jesus Christ of Latter-Day Saints (FLDS), hata hivyo Blackmore alifukuzwa kutoka FLDS mwaka 2002.

Kuoa wanawake wengi ni haramu chini ya sheria za Canada, Palisi nchini Canada walianza kuchunguza dhehebuhilo mnamo miaka ya 1990.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents