Aliyepanga njama ya wanariadha kutumia dawa za kusisimua misuli Urusi na badaye kufichua siri hiyo, yupo mafichoni Marekani

Aliyepanga njama ya wanariadha kutumia dawa za kusisimua misuli Urusi, Grigory Rodchenkov, alifanya mahojiano na BBC wiki hii akiwa amevaa kofia hadi machoni iliyotengenezwa kwa mabua na kujifunika nyuso kwa kitambaa cheusi. Sasa hivi yuko mafichoni Marekani baada ya kufichua yote kwa Shirika la kimataifa la kukabiliana na dawa za kusisimua misuli michezoni WADA, bila shaka hiyo ilikuwa tahadhari ya kulinda maisha yake. Matt Majendie ameelezea sababu ya kujitokeza kwa namna hiyo.

Ni watu kidogo sana wanaofahamu alipo Bwana Grigory Rodchenkov. Hata wakili wake Jim Walden, hajui mteja wake amejificha wapi. Lakini maafisa wa Urusi wanamsaka kwa udi na uvumba.

Marekani ilipowafurusha wanadiplomasia 60 wa Urusi nchini humo, kama hatua ya kupinga kutiliwa sumu kwa Sergei Skripal huko Salisbury March 2018, Walden alifahamishwa kwamba kuna baadhi ya majasusi wa Urusi waliokuwa wanamfuatilia mteja wake.

“Tulichofahamu kutoka kwa Shirika la upepelezi la Marekani ni kwamba watatu kati ya raia wa Urusi waliofurushwa Marekani walikuwa wameletwa na Urusi kujaribu kumtafuta Dkt Rodchenkov. Tuliona picha za watu hao. Kwa hiyo tishio dhidi ya Dkt Rodchenkov ni kweli.”

Grigory Rodchenkov in 2007
Grigory Rodchenkov mwaka 2007

Mkuu wa maabara ya kupima matumizi ya dawa za kusisimua misuli Moscow, Rodchenkov ndiye aliekuwa mpangaji wa njama hiyo kwa Urusi huko London 2012 pamoja na michezo ya msimu wa baridi iliyofanyika Sochi miaka miwili baadae.

Lakini Wada ilipoanzisha uchunguzi 2015 iligundua jinsi maabara hiyo ilivyoshindwa kufanya vipimo stahiki na uharibifu uliofanyika kwa sampuli 1,417 na mkuu wa maabara akakimbilia Marekani. Na kama alivyoelezwa katika makala iliyoshinda Tuzo la Oscar Icarus, alikuwa mfichuzi wa ngazi ya juu kukiri yote.

Kwa baadhi ya raia wa Urusi alikuwa msaliti. Rais Vladimir Putin amekuwa akisema kwamba yuko “chini ya udhibiti wa huduma maalum ya Marekani”, na kumuelezea kama hayawani ambaye bila shaka ana matatizo”.

Lakini kwa sasa, Rodchenkov anaishi akisimulia kilichotokea. Kama Walden anavyosema: “Ameishi maisha mara kadhaa ndani ya mwili mmoja. Ni jambo la kipekee kuona vile ambavyo amekuwa na mahusiano mazuri, mwenye bahati na kwa kiwango fulani amefanikiwa kunusurika yote tofauti na ilivyotarajiwa.”

Taaluma ya Rodchenkov nchini Urusi katika maabara za kupanga njama ya matumizi ya dawa za kusisimu misuli ilionekana kufikia ukingoni mwaka 2011 alipokamatwa na kushutumiwa kwa ulanguzi wa dawa za kulenya pamoja na dada yake, Marina.

Agizo la kukiri makosa kwenye kesi hiyo, anasisitiza lilifanya mambo kuwa mabaya kiasi cha kujaribu kujitoa uhai.

Halafu akafungiwa kwa taasisi kadhaa za matatizo ya akili na kupewa dawa zinazoathiri akili mara kadhaa”, kulingana na Walden, ambaye anasema maisha yake yaliokolewa kwa mwaliko tu kutoka Uingereza.

Grigory Rodchenkov
Grigory Rodchenkov akizungumza na mwanahabri wa BBC Dan Roan Februari 2018

Kwa maandishi, bado alikuwa msimamizi mkuu wa maabara kwa michezo ya Sochi 2014, kwahiyo aliaalikwa London 2012, kujiunga na msimamizi mkuu wa vipimo vya wanariadha David Cowan katika maabara ya Harlow, kwa michezo ya 2012.

Ulikuwa mkutano wa kijasusi ambapo hangeweza kukosekana na mwaliko huo ulikuwa ni wake peke yake, kwahiyo akaachiliwa huru na kufutiwa rasmi makosa yote dhidi yake.

Cowan hakufurahishwa na hatua hiyo – na kama wengine wengi, alikuwa na wasiwasi na wafanyakazi wenzake wa Urusi – lakini hakuwa na uwezo wa kufanya lolote. “Kwasababu alikuwa mwanachama wa tume ya matibabu ya kamati ya olimpiki, maabara ilihitajika kumpa taarifa ya kile kinachoendelea,” anasema. “Yeye aliruhusiwa kuona kila kitu kinachoendelea.”

Hadi kufikia kiwango hicho, dawa iliyokuwa inatumiwa na wanariadha wengi wa Urusi ni ile ya kumeza ya turinabol, iliyotengenezwa kama sehemu ya mpango mwengine wa kusisimua misuli unaosimamiwa na serikali mashariki mwa Ujerumani miaka ya 1970.

Tayari wakati wa safari yake, Rodchenkov ilijua kuna uwezekano mkubwa Urusi ikanaswa, sio kwenye michezo yenyewe lakini kupitia mchakato wa kupimwa mara kadhaa kama hatua mpya.

Na sasabu iliyomfanya ajue hilo ni kwamba alikuwa amebaini vipimo hivyo na kuchapisha matokeo yake 2011, licha ya kufahamu fika kwamba hilo lilikuwa na uwezo wa kugharimu pakubwa Urusi siku za usoni. Lakini kwanini alifanya hivyo bado limesalia kuwa fumbo.

Na wakashikwa. Kati ya wanariadha 140 waliondolewa kwenye mashindani la London 2012, zaidi ya theluthi moja walikuwa Warusi. Inawezekana wengine zaidi wakatangazwa kabla ya Agosti 6, miaka minane baadae tangu kumalizika kwa michezo ya London. Na baada ya hapo, hatua ya kupimwa tena itakuwa imefikia ukomo.

Lakini 2012, Rodchenkov alikuwa ameanzisha matumizi ya dawa mpya inayotumika katika mifugo ambazo hakuna inayoweza kubainika katika hatua ya kupimwa kwa muda mrefu.

Katika michezo ya msimu wa baridi ya Sochi, wanariadha walikunywa dawa hiyo na pombe kusaidia mmeng’enyo wake wanaume wakanywa aina yao na wanawake aina yao. Dawa hizo ziliingia dani ya mwili kupitia seli za mashavuni kwasababu waliizungusha ndani ya mdomo mfano wa kusukutua kabla ya kuitema.

Grigory Rodchenkov examining a tamper-proof urine sample bottle in the documentary, Icarus
Rodchenkov akichunguza chupa ya sampuli ya mkojo iliyobadilishwa katika makala ya ‘Icarus’

Ikiwa kabla Urusi ilitegemea kuwapa dawa wanariadha wake wakati wa mazoezi, safari hii walikunywa wakati wa michezo vilevile.

Kama inavyoelezwa kwenye makala ya, Icarus, sampuli za mikojo michafu ya Warusi zilitolewa kutoka maambara ya Wada kupitia kishimo kilichopo ukutani na kubadilishwa kwa mikojo mingine misafi iliyoingizwa kwenye maabara hiyo kupitia njia hiyo hiyo.

Cha msingi ilikuwa ni mbinu iliyotumiwa na huduma ya usalama ya Urusi, kufungua vichupa vilivyo na sampuli kwa vipade vidogo vya chuma. Ulikuwa ni udanganyifu ngazi ya olimpiki, na mwenyeji, furaha aliyokuwa nayo Putin, alitia kibindoni medali 33.

Rodchenkov – ambaye alikuwa amefungwa gerezani miaka mitatu iliyotangulia tu – alipewa Tuzo ya Urafiki na serikali ya Urusi.

Lakini nyakati hizo nzuri zilikuwa fupi mno. Mambo yalianza kumwendea mrama asante kwa mfichuzi wa Urusi, uchunguzi uliofanywa na runinga moja Ujerumani 2014 pamoja na uchunguzi wa Wada, ambali 2015 likaishutumu Urusi rasmi kwa kusimamia matumizi ya dawa kusisimua misuli.

Kwa wiki kadhaa baada ya kuchapishwa kwa ripoti ya Wada, Rodchenkov anasema alidokezwa na rafiki yake anayefanyakazi Kremlin kwamba maisha yake yako hatarini kwa hiyo alifungasha nguo zake, akambusu mke wake na kuwaaga watoto wake na kuhamia Marekani.

Na kuanza kutoa ushirikiano kwa uchunguzi mwingine zaidi, ukiwemo ule wa wakili wa Canada Richard McLaren ambao ulielezea kwa kina udanganyifu uliofanywa na Urusi wakati wa mashindano ya Sochi na hatimae wanariadha wa Urusi wakapigwa marufuku pamoja na wanyanyuaji uzani kushiriki michezo ya Rio.

Pia unaweza kusoma:

 

Na tangu mwaka huo, wanariadha 28 waliopigwa marufuku kwasababu ya ushahidi ulitolewa na Bwana Rodchenkov marufuku zao zimebatilishwa na Mahakana ya usuluhishi wa mizozo katika michezo kwasababu ya ukosefu wa ushahidi wa kutosha, lakini kuna ishara kidogo sana ya Urusi kujitakasa kwa kitendo chake.

Desemba, Urusi ilipigwa marufuku kushiriki kwa mashindano yote makubwa ya michezo kwa miaka minne kwasababu ya kuingilia data za maabara.

Rufaa ya Urusi dhidi ya umauzi huo wa Novemba huenda ukatoa mwanga zaidi kwa kilichotokea kwenye maabara hatua iliyo na uwezo wa kutoa ushahidi zaidi kuthibitisha madai ya Rodchenkov.

Ikiwa Rodchenkov angesalia Urusi, Walden anasema anajua vile ambavyo suala hilo lingeshughulikiwa.

Katika kipindi cha wiki mbili tu mwaka 2016, muda mfupi baada ya mteja wake kuondoka nchini humo, wakuu wawili waliokuwa wanasimamia Shirika la kukabiliana na dawa za kusisimua misuli Urusi (Rusada), Vyacheslav Sinev na Nikita Kamaev, wote walikufa katika hali ya kutatanisha.

Kulingana na Walden, tishio kwa maisha ya Rodchenkov bado lipo juu hata baada ya wanadiplomasia wa Urusi kufurushwa Marekani.

“Mradi rais Vladimir Putin ndie anayeongoza magenge ya uhalifu Urusi, hakuna afueni yoyote kwa Dkt Rodchenkov,” Walden anasema. “Anastahili kuwa makini kwa kila hatua anayopiga njiani.”

Grigory Rodchenkov appears by videolink at a Foundation for Sports Integrity conference in May 2018
Grigory Rodchenkov alipojitokeza kwa njia ya video katika mkutano wa uadilifu wa michezo Mei 2018

Rodchenkov hafichi kwamba yeye mwenyewe alikunywa dawa hizo kipindi cha taaluma yake kama mwanariadha.

Aliyekuwa rais wa Wada John Fahey aliwahi kusema kuhusu wakati wa matembezi ya maabara ya Uingereza na Rodchenkov. Walipopita picha za wanariadha watatu akiwemo Rodchenkov wakati huo mwanasiasa wa Urusi alishika kila mmoja wao huku akisema, “Hawa ni watumiaji wa dawa za kusisimua misuli.”

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW