Habari

Ali Choki akataa kuhusishwa kwenye tuzo za Kili 2013

Mkurugenzi wa bendi ya Extra Bongo Ali Choki kwa mara nyingine amekataa kuhusishwa kwenye tuzo za Kili kwa kile anachodai ni kutokuwa na imani nazo.

KIMO3
Ali Choki ametoa msimamo huo kwa bongo5 na kuelezea jinsi anavyouchukulia mchakato wa tuzo hizo.

“Mwaka jana nilitangaza kuwa sitaki tuzo hizo lakini wakatuingiza kwa nguvu,nilienda baraza la sanaa taifa “BASATA” kutoa angalizo kuwa sihitaji tena na kuomba mwaka unaofuata waniepuke kabisa,” amesema Choki.

“Hizi tuzo zina mapungufu makubwa sana huwezi kuwaweka Diamond,Ali Choki ,Gurumo na Mzee Yusuf kwenye uimbaji bora au unawaweka Linah, Mbutu na Khadija Kopa itakuwa kuna watu ambao hawatendewi haki.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents