Mitindo

Ally Daxx: Model wa Tanzania aliyewahi kufanya matangazo ya magari ya kifahari ya Aston Martin

Ally Daxx, model anayefanya kazi na agency ya Ice Model Management jana alifunguka kwenye show ya Clouds E ya Clouds TV na kutoa exclusive kibao ikiwemo kufanya matangazo ya magari ya kifahari duniani, Aston Martin.

550891_533924536621510_558447712_n
“Nimefanyakazi Ice Model management kwa muda miezi kumi sasa na nimefanya kazi nyingi . Baadhi yake ni kufanya matangazo ya magari kama Aston Martin na Alfa Romeo. Pia nimefanya matangazo ambayo yameingia kwenye magazine kubwa sana kule bondeni kama Drum magazine na People magazine,” alisema.

197788_641146415899321_1968420997_n

Akizungumzia utofauti wa tasnia ya mitindo hapa Tanzania na Afrika Kusini, Daxx alisema:

“Ni wazi kwamba South Africa mambo yapo so professinal zaidi ya bongo,agency inatakiwa kumsimamia model vizuri hadi kumpa mipaka ili aweze kufanya kazi vizuri. Mfano my agency inatoa support kwa model wao kwa kumtafuta special apartment za kuishi na kulipa 50% ya rent na model analipa 50%. Hakuna mambo ya kusumbuna kwenye malipo, kila kitu kinaenda according to contract yako ilivyo, tofauti na bongo, kulipana pesa baada ya kazi hapa bongo ni hadi mkimbizane au mgombane kwenye simu.”

480974_547204618626835_1977420793_n

Akiongelea michongo yake ya baadaye, Daxx amesema:

“Nimepata nafasi ya kutuma picha zangu kwenye agency moja huko New York, so wamekuwa interested na mimi. Nasubiri utaratibu ukamilike, then I will be on to New York kuendeleza mipango yangu na this career.”

225542_612518365428793_1369407267_n

Clouds E huruka kupitia Clouds TV kila siku saa mbili usiku.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents