Michezo

Ally Mayay ajinadi kwenye utawala bora kampeni za TFF (Video )

Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) na klabu ya Dar es salaam Young Africans, Ally Mayai ‘Tembele’ amezindua rasmi kampeni za kuwania nafasi ya  Urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), leo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Ramada Posta jijini Dar es Salaam, huku akitaja vipaumbele kadhaa.

Mayay amesema kuwa endapo atapata nafasi ya kuwa rais wa TFF  anaahidi kuwa muadilifu na kuhakikisha kuna kuwepo na misingi ya utawala bora. Kwa kuhakikisha kuwa na uwazi, uwajibikaji, kufuatasheria,kufuata taratibu na kutokuwa na upendeleo hivyo anaaminikuwa ana uwezo wa kusimamia hilo.

Mchambuzi huyo wa soka nchini Mayay ameongeza kuwa  katika upande wa soka la ufukweni tayari Tanzania ina bahati ya kuwa na eneo kubwa la bahari na hata kwa upande wa soka la wanawake na hivyo kilichobaki ni uwekezaji hasa kuheshimu misaada inayotolewa na wafadhili na kusimamiwa madhubuti swala ambalo yeye anaamini anaweza.

Kwakuwa Tanzania hakuna ligi ya wanawake lakini bado timu ya wanawake inaonyesha uwezo katika mashindano mbalimbali na kufanikiwa kushiriki fainali za AFCON hivyo kinachotakiwa ni kuhakikisha kunakuwa na Ligi imara ya wanawake.

Lakini pia amezungumzia fainali za vijana walio na umri chini ya miaka 17 ambazo Tanzania ndiyo mwenyeji, Ally Mayay amesema kuwa katika kuelekea michuano hiyo atatumia wataalamu katika kila sehemu itakayo hitajika kufanya hivyo ili kuhakikisha sio tu kutangaza mpira wa miguu bali pia kuitangaza nchi lakini pia kuhakikisha mradi wa vijana wa 2013  waliopo katika kituo cha Alliance  atahakikisha kunakuwa na mashindano ili kuwapata vijana wa kuwaongeza

By Hamza Fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents