Burudani

Ally Nipishe aeleza kwanini nyimbo zake hazifanyi vizuri

Msanii wa muziki aliyewahi kufanya vizuri na wimbo ‘My’, Ally Nipishe amefunguka kuzungumzia kitu ambacho kinafanya nyimbo zake nyingi za hivi karibuni zishindwe kufanya vizuri.

Ally Nipishe

Muimbaji huyo ameachia nyimbo nyingi hivi karibuni ambazo zimeshindwa kufanya vizuri.

Akiongea na Bongo5 Jumamosi hii, Ally amedai nyimbo zake nyingi zimeshindwa kufanya vizuri kutokana na kukosa usimamizi.

“Unajua muziki umebadilika sana, unahitaji usimamizi mkubwa sana tofauti zamani,” alisema Ally Nipishe.”Kusema kweli ngoma zangu za zamani kama ‘My’ ilipata usimamizi mzuri sana tofauti na nyimbo zangu za hivi karibuni ingawa zinasimawiwa lakini bado hatujafika sehemu ambayo tunahitaji kufika,”

Muimbaji huyo ambaye yupo chini ya Papa Misifa, amedai kwa sasa anajipanga zaidi ya management yake ili kuhakikisha anarudi kwenye chati kama zamani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents