Ally Remtullah na Diana Magessa kuonesha mavazi Washington DC

Tanzania’s top designers , Ally Rehmtullah na Diana Magessa wanatarajiwa kuwasha moto katika maonyesho ya mavazi ya Mitindo Nite 3, USA yanayofanyika kila mwaka, Jumamosi ya Thanksgiving jijini Washington DC.

Maonesho hayo yanaandaliwa na designer Ma Winny na J &P.

Mmoja wa waratibu wa maonyesho hayo ya mitindo Bwana Dickson Mkama aka DMK amesema mwaka huu wamejiandaa kwa show ya aina yake ambayo mbali na Tanzania kuna madesigner kutoka nchi mbali mbali za Africa na Caribbean pamoja na super models 16 kutoka kampuni ya IHI Modeling Agency.

Kwa upande wa burudani mwanamuziki mahiri wa kike Hafsa Kazinja atakuwepo kuangusha show ya nguvu katika maonyesho hayo yaliyoandaliwa na makampuni ya J&P, DMK Promotions na Northern Zone Ent.

MC wa shughuli hiyo anatarajiwa kuwa Sunday Shomari wa Voice of America.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents