Diamond Platnumz

Ally Remtullah na Sammy Cool kuungana na Diamond kwenye usaili wa video models

Jumamosi hii Diamond atafanya usaili wa kutafuta models takriban 20 wa kike na wa kiume watakaoonekana kwenye video yake mpya.

Usaili huo utafanyika Nyumbani Lounge huku majaji wakiwa yeye mwenyewe Diamond, mbunifu wa mitindo wa kimataifa Ally Remtullah mwalimu wa dansi (choreographer) Sammy Cool na mwandishi wa blog Missie Popular.

Video hiyo itafanyika nchini na nje ya nchi huku kampuni ya I-View Media chini ya Raqey Mohamed ikihusika katika kuitengeneza.

Katika interview aliyoifanya hivi karibuni kupitia kipindi cha Hot Mix cha EATV, Diamond alisema watu wengi wamekuwa wakimpigia simu kutaka kushiriki bure kwenye video zake lakini amesema ameamua kufanya usaili ili kupata models atakaowalipa ujira mzuri.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents