Michezo

Almunia Aililia Arsenal

 

Kipa wa Arsenal, Manuel Almunia amesikitiswa na kitendo cha kocha mkuu wa timu hiyo, Arsene Wenger, kutaka kumsajili kipa wa Fulham Mark Schwarzer.

Almunia aliyekuwa nahodha wa timu hiyo wakati ilipotoka sare ya 1-1 na Liverpool wikiendi ilyiopita amesema ingawa kocha wa timu yake anamatarajio ya kumsajili kipa mya kutoka Fulham yeye atajitahidi kuyafnya yale yanyohitajik kwake kutoka meneja wa Arsenal pamoj na mujibu wa mkataba.

Kipa huyo mwenye uraia wa Hispania amesema hafikirii wala kuona maisha mengine kisoka mbali na Arsenal,na kuongezea kwamba iwapo kipa Mark Schwarzer atatua uwanja wa soka wa Emirates Stadium, basi atahitaji kuzungumza na Wenger.

“Itakua vigumu kwangu mimi kucheza kwenye timu nyingine hapa England kama sio Arsenal,au hata kuichezea Hispania itakua ngumu sana. Nina miaka 33 sasa,hivyo bado nina miaka michache sana ya kucheza soka,nataka kufurahia sana kipindi kilicho baki. Mimi ni kipa ambaye anapenda kucheza kila mara. Kitu pekee ninachotakiwa kufanya ni kuongeza juhudi kwa kuwa nina mkataba hapa na kuakikisha nafanya kile ambacho kocha anatakam alisema Almunia

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents