Habari

Amina, Zitto ruksa !

Waheshimiwa wabunge, Amina Chifupa wa CCM na Zitto Kabwe wa CHADEMA ni ruksa kwao kujivunia uhuru wao binafsi kama katiba inavyosema

Na Usu-Emma Sindila, Jijini



Waheshimiwa wabunge, Amina Chifupa wa CCM na Zitto Kabwe wa CHADEMA ni ruksa kwao kujivunia uhuru wao binafsi kama katiba inavyosema.


Akizungumza na Alasiri leo asubuhi, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CHADEMA, Bw. Erasto Tumbo, amesema anawashangaa watu wanaolivalia njuga suala kwamba wabunge hao vijana wana uhusiano wa kimapenzi na kusahau katiba ya nchi inasemaje kuhusiana na uhuru wa mtu binafsi.


`Ninawashangaa hawa watu wanaolivalia njuga suala hili� yawezekana hawajui na hawajawahi kusoma katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kipengele kinachozungumzia uhuru wa mtu binafsi na maisha yake,` akasema Bw. Tumbo.


Kwa mantiki hiyo, Bw. Tumbo amesema kuwa CHADEMA haiwezi kujiingiza kwenye masuala binafsi ya wabunge hao kwani wana ruksa ya kufanya watakacho ilimradi hakiingilii masuala ya chama.


Akasema mbunge Zitto hawezi kuchukuliwa hatua yoyote na chama chao kwa sababu, CHADEMA haiwezi kushughulikia tuhuma zozote ambazo ni za kizushi.


Amesema hivi sasa, Bw. Zitto mwenyewe hajalifikisha suala hilo mbele ya chama ili liweze kushughulikiwa na hiyo ni sababu nyingine inayowafanya wasione sababu yoyote ya kujadili tuhuma za kizushi mbele ya vikao vyao vya chama au kamati.


`Ni mambo yanayoonekana wazi kuwa ni ya kuzushwa� isitoshe, yanahusiana zaidi na watu binafsi na wala siyo chama. Chama chetu kinazingatia uhuru binafsi wa kila mtu,` akasema Bw. Tumbo.


Mapema wiki iliyopita vyombo vya habari mbalimbali vilinukuliwa vikisema kuwa Mheshimiwa Amina Chifupa amelimwa talaka na mumewe Mohamed Mpakanjia baada ya kubainika kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mheshimiwa mwenzie, Bw. Zitto Kabwe wa CHADEMA.


Hata hivyo, ilidaiwa baadaye kuwa huo ni uzushi uliotengenezwa� na wapinzani wa Amina ndani ya CCM ili kumtibulia mipango yake ya kuwania uenyekiti wa umoja wa vijana ndani ya CCM.


Source: Alasiri

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents