Umbea

Amini amefukuzwa THT, anataka kujitoa ama yote ni uzushi?!


Kuna habari kwamba mwanamuziki wa kizazi kipya Amini Mwinyimkuu ‘Amini’ amejitoa katika kundi la Nyumba ya Vipaji Tanzania THT, huko wengine wakisema kwamba msanii huyo anaweza akafukuzwa kutokana na utovu wa nidhamu…Nani yupo sahihi? Ama yote ni mbinu ya kujipandisha chati katika habari?

Baada ya kumtafuta Amini, msanii huyo alifunguka na Bonog5.com na kusema kwamba jambo hilo ataliweka wazi hivi karibuni pindi atakapofanya uzinduzi wa nyimbo yake mpya itakayokwenda kwa jina la Ni Wewe. Aliongeza kwa kusema kwamba kuhusu yeye
na THT, bado itabakikuwa kitendawili kwakuwa muda wa kuliongelea haujafika, kwani anategemea kila kitu atakiweka hadharani siku hiyo.

Kumbuka amini ni miongoni mwa wasanii wakubwa wa THT, ambaye alishawahi kuwatungia wasanii mbalimbali wa kundi hilo akiwemo Mwasiti na wengine kuwapa ushauri na hata kuwasaidia katika kutafuta sauti ya wimbo.

Pia alishawahi kuwa na uhusiano na mwanamuziki mwenzake wa kundi hilo Linah.

Swali watu bado wanajiuliza juu ya kuhama kwake THT, ni kweli? Kwa nini? Wapi anatarajia kwenda?

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents