Moto Hauzimwi
TECNO Spark 2

Amitabh Bachchan agonga miaka 75 na mafanikio lukuki

Ukiachia uigizaji wake mahiri katika filamu pia staa huyo mkubwa dunia kutoka nchini India Amitabh Bachchan, amejawa na uwezo ikiwemo utayarishaji filamu , kuimba muziki, kuandika mashahiri na utangazaji wa tv.

Siku ya leo ni siku muhimu kwa muigizaji huyo anayetiza miaka 75 katika maisha yake na bado amekuwa mtu mwenye kuhitajika katika sekta ya filamu dunia hii tangu miaka ya 70 alivyoingia rasmi katika game.

Pia muigizaji huyo ana utajiri wa kiasi cha dola milioni 400 za Kimarekani sawa na kiasi cha Shilingi bilioni mia tisa za Kitanzania hii ni kwa muijibu wa ripoti iliyotolewa mwezi Mei mwaka huu, ikiususha nyumba zake, magari ya kifahari takribani 15 na mali zingine huku akimzidi utajiri shwahida wake Shahrukh Khan.

Vile vile amewahi kushinda tuzo za kadhaa za filamu ikiwemo Padma Vibhushan 2015, Padma Bhushan 2001 na Padma Shri 1984 huku akishiriki filamu zaidi ya 100.

“The affection of greeting for the 75th, displayed over several mediums, overwhelms me .. a thank you shall never be enough,” ameandika msanii huyo nguli katika filamu kwa mashabiki zake.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW