Amka mtanzania ya Music Lab kufanyiwa video Jumapili hii


Ule wimbo wa Hip Hop uliofanywa na takriban rappers saba nchini, unafanyiwa video Jumapili hii.

Wimbo huo uliowakutanisha Songa, Zaiid, P the Mc, Wakazi, One incredible, Stereo na Nikki mbishi una lengo la kuwakumbusha watanzania kuwajibika katika maisha yao na kuacha kulalamika.

Kutokana na umuhimu wa mada hiyo kwa jamii ya kitanzania sasa uongozi wa studio hiyo umeamua kuifanya kuwa project yenye nyimbo kumi.

“AMKA MTANZANIA: well..project hii sasa imekuwa kubwa. Sasa inakuja kama mixtape itakayokuwa na nyimbo 10 zote zikiwa na nia ya kumhamasisha mtanzania. Leo (June 8) katika hatua kubwa ya nyimbo hiyo, Nikki mbishi aka Baba Malcom amejumuika katika kutia vocals kwenye wimbo huo.

Halafu kijana mwenye kipaji kikubwa kwenye gitaaa….anafahamika kama Imma akaingiza distortion ya gitaa pale ya ajabu.” MLAB wameandika katika ukurusa wao wa Facebook.

Wameongeza. “Amka Mtanzania: nguvu zako, juhudi zako ndio mtaji. Usilalamike sana haibadili hata nukta kwenye maisha yako. Kama ni wakusoma soma sana kabla ya gambe. Sista duu kumbuka utajikomboa si kwa kubebwa, kama ni mbunge… wajibu wako unaufahamu, kama ni kiongozi wa dini, simamia amani, kama ni mjasiriamali basi hakikisha unakomaa. Kama upo nje ya nchi kumbuka kuwekeza nyumbani, huwezi jua.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents