Habari

Amkata mumewe uume

Maria Luambano, mwanamke mwenye umri wa miaka 43, mkazi wa kijiji cha Likuyufusi, Wilaya ya Songea Vijijini mkoani Ruvuma, ametiwa mbaroni kwa tuhuma za kuukata uume wa mume wake baada ya kumkuta akiwa na kondomu.

Na Gideon Mwakanosya, PST Songea



Maria Luambano, mwanamke mwenye umri wa miaka 43, mkazi wa kijiji cha Likuyufusi, Wilaya ya Songea Vijijini mkoani Ruvuma, ametiwa mbaroni kwa tuhuma za kuukata uume wa mume wake baada ya kumkuta akiwa na kondomu.


Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Bw. Falhum Mshana, alisema tukio hilo lilijiri Julai 27, mwaka huu, saa 5:00 usiku kijijini hapo.


Kamanda Mshana alisema mwanamke huyo, alimkata mumewe, Bw. Ferdnand�Mwingira (45) sehemu za siri kwa kutumia kitu chenye ncha kali.


Alisema mwanamke huyo alifanya kitendo hicho kwa madai ya kuchoshwa na tabia ya mume wake ya kufanya mapenzi na wanawake wengine.


Kamanda Mshana alisema siku hiyo, mwanaume huyo alifika nyumbani kwake akitokea mjini Songea akiwa amebeba vitu mbalimbali kikiwemo chakula na kupokelewa mzigo huo na mke wake.


Alisema baadaye, mke wake aliona kondomu ya kiume ikiwa chini ya godoro la kitanda chao na alipomhoji mume wake mpira huo ni wa nani, alimjibu kuwa alipatiwa na washauri nasaha wa ugonjwa wa Ukimwi mjini Songea.


Baada ya mahojiano hayo, Kamanda alisema wote waliondoka nyumbani na kwenda kunywa pombe za kienyeji lakini wakiwa njiani kurejea kwao, mke wake aliendelea kumhoji kuhusu kondomu hiyo.


Alisema katika mabishano hayo, ghafla mke wake alimrukia mume wake na kumdondosha chini kisha akamvua suruali na kumkata uume wake kwa kutumia kitu chenye ncha kali.


Kwa mujibu wa Kamanda Mshana, �majeruhi huyo kwa sasa amelazwa katika hospitali ya Misheni ya Peramiho akiendelea kuuguza jereha hilo huku polisi wakiendelea na uchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hilo.


Alisema baada ya upelelezi kukamilika, mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayomkabili.


Souce: Nipashe

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents