Michezo

Amunike aishitaki TFF mbele ya FIFA, abeba hoja hii ”Ni sahihi mtu kutolipwa pesa baada ya kufanya kazi ?”

Aliyewahi kuwa Kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania, Emmanuel Amunike amelishtaki Shirikisho la soka nchini TFF, kwa shirikisho la Soka Duniani FIFA kwa madai ya kutolipwa stahiki zake.

Image result for Amunike

Amunike alivunjiwa mkataba wake na TFF tangu mwezi Julai mwaka huu kutokana na matokeo mabovu iliyoipata timu ya Tanzania kwenye fainali za mataifa ya Africa (Afcon) 2019.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mitandao ya completesports.com na punching.com, Amunike ameamua kupeleka shauri hilo FIFA ili waweze kulitatua.

“Nimewasiliana na FIFA juu ya hilo jambo. Sio suala la kupigia kelele, lakini nina imani watalitazama na kuamua kama ni sahihi mtu kutolipwa baada ya kufanya kazi.” Alisema Amunike.

Emmanuel Amuneke aliyekuwa kocha msaidizi wa  Super Eagles ameiwezesha Tanzania kutinga michuano ya AFCON kwa mara ya kwanza baada ya kupita miaka 39, hata hakufanikiwa kuchomoza na ushindi katika michezo yake yote.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents