Habari

Amuua kwa kumchoma kisu mvulana wa miaka 17 kwa kusikiliza muziki wa Hip Hop, Mahakama yamuachia huru

Kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Michael Adams (27) kutoka nchini Marekani ameachiwa huru na Mahakama mjini  Peoria Ave, Arizona, Marekani,  baada ya kukutwa bila hatia kwenye kesi yake ya tuhuma za mauaji ya kijana mwenye umri wa miaka 17, Kwa kumchoma kisu hadi kufariki kwa sababu ya kusikiliza muziki wa Hip Hop.

Elijah na Michael Adams

Kwa mujibu wa maelezo ya awali yaliyotolewa Alhamisi iliyopita na Polisi mjini Peoria Ave,  Yalieleza kuwa mtuhumiwa huyo alikiri kufanya tukio hilo na ameeleza sababu za kufanya hivyo ni kuwa marehemu alikua anasikiliza muziki wa Hip Hop kwenye gari lake jambo lililomfanya ajione hayupo salama na kuanza kumvamia kwa kumchoma kisu.

Taarifa za Michael Adams kuachiwa huru zimetangazwa na Mahakama mjini humo, Mapema siku ya leo, Hii ni baada ya gereza la Arizona State Complex kutoa taarifa kuwa mtuhumiwa huyo aliyekuwa anashikiliwa kupisha uchunguzi, ameachiwa huru baada ya kukutwa bila hatia mahakamani.

Mtuhumiwa alijiona hayuko salama baada ya kuona kijana huyo akipiga muziki huo kwa sauti huku akimsongelea na gari lake, Jambo ambalo amekiri kuwa aliona ni vyema ajihami kuliko kushambuliwa. Hivyo Mahakama imechukuliwa kama tahadhari kwa mtuhumiwa huyo kujihami.“Imeeleza taarifa iliyotolewa na Mahakama juu ya hukumu hiyo.

Tayari jamii ya watu weusi na wanaharakati wa ubaguzi wa rangi nchini humo, Wameanzisha kutumia Hashtag ya #JUSTICEFORELIJAH kutaka mahakama itende haki bila kujali rangi.

Kwenye video hiyo, Inaonesha mtoto huyo akiwa anasikiliza muziki na akishuka kwenye gari huku akisikiliza muziki kwa sauti na baadae akishuka na kuingia kwenye duka la nguo, Kisha Adams akamfuata na kumvamia.

Chanzo: https://www.azcentral.com/story/news/local/peoria-breaking/2019/07/05/deadly-peoria-stabbing-suspect-michael-paul-adams-says-he-threatened-teens-music/1657727001/

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents