Amuua Mkewe kwa kumchoma visu

Mauaji ya kinyama yametokea usiku wa kuamkia leo Jijini baada ya mwanaume mmoja kudaiwa kumuua mkewe kwa kumcharanga visu mwilini, kwa madai yake kuwa eti, amekerwa na tabia ya kugawa penzi ovyo kwa wanaume wengine.

Mauaji ya kinyama yametokea usiku wa kuamkia leo Jijini baada ya mwanaume mmoja kudaiwa kumuua mkewe kwa kumcharanga visu mwilini, kwa madai yake kuwa eti, amekerwa na tabia ya kugawa penzi ovyo kwa wanaume wengine.

Mwanaume anayedaiwa kutenda unyama huo mishale ya saa 7:00 usiku wa ametajwa kwa jina kuwa ni Bw. Selemani Omari, (46) mkazi wa Mbagala Charambe, eneo la Kwa Padri.

Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Temeke, Emmanuel Kandihabi, ndiye aliyeelezea tukio hilo na kudai kuwa Omari, anadaiwa kumuua mkewe ajulikane kwa jina la Bi. Halima Mohamedi (36) kwa kumchoma visu mwilini na kumfanya apoteze maisha papo hapo.

Akasema baada ya kumuua mkewe, Omari alijaribu kujiua mwenyewe kwa kunywa sumu ambayo hadi sasa haijafahamika ni ya aina gani. Akasema mbali ya kunywa sumu, pia Omari alikuwa ameshaacha ujumbe unaosomeka kuwa.

“Mimi Seleman nimefanywa vibaya na mke wangu Halima kwa kufanya mapenzi na watu wengine” hata hivyo, Kamanda Kandihabi amesema hadi sasa, hali ya Omari ni mbaya na kwamba bado amelazwa katika Hospitali ya Temeke kwa matibabu zaidi.

Amesema mwanaume huyo ambaye yupo chini ya ulinzi mkali wa Polisi, atafikishwa mahakamani na kufunguliwa kesi ya mauaji mara baada ya upelezi kukamilika.

Aidha amesema mwili wa marehemu Halima umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali hiyo ya Temeke.

 

 

 

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents