Tupo Nawe

Amuua mtoto wa jirani yake kwa kumkata panga kichwani, kisa wivu wa mapenzi

Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga linamshikilia mwanadada, Paskazia Andrew Sindano (17) kwa tuhuma za mauaji ya mtoto Kashindye Mgemagiko (03) kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi.

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga, Simon
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga, Simon Haule 

Taarifa iliyotolewa Jana Februari 17, 2019 na kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga, Simon Haule imeeleza kuwa tukio hilo lilitokea juzi Ijumaa saa 12 jioni katika kitongoji cha Emalaupena kijiji cha Misayu kata ya Ubagwe, halmashauri ya wilaya ya Ushetu.

Chanzo cha tukio hili ni wivu wa kimapenzi kwa kuwa mama wa mtoto aliyeuawa inasemekana alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mume wa Paskazia na kupelekea kuzaliwa mtoto huyo,” amesema Kamanda Haule.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa mbinu iliyotumika ni ya kumkata panga kichwani nje ya nyumba yake.

Kamanda Haule amesema kuwa kwa sasa mwili umehifadhiwa na mtuhumiwa  atafikishwa mahakamani mara moja.

Kwa upande mwingine, Kamanda Haule amewataka wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi na badala yake wapeleke malalamiko, kero na migogoro yao katika ofisi za serikali ya kijiji au mabaraza ya wazee ili kuepuka vitendo vya kikatili.

Chanzo : https://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/kuua-mtoto-wa-miaka-mitatu-kwa-kumkata-panga-kichwani/1597296-4986684-efs3vm/index.html

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW