ANC yampa saa 48 Rais Zuma kung’atuka

Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma amepewa saa 48 awe amejiuzulu, katika nafasi hiyo.

Hatua hiyo inakuja baada ya mazungumzo yaliyofanywa na chama tawala cha nchini, ANC kwa muda.

Taarifa zinaeleza kuwa ANC walituma watu wawili nyumbani kwa Rais Zuma, Pretoria kumfikishia ujumbe wa chama kwamba anatakiwa ajiuzulu mwenyewe au chama kimng’oe madarakani.

Hatua hii ya ANC inaonekana ndio njia rahisi zaidi ya chama hicho kumng’oa Rais Zuma madarakani badala ya kusubiri utaratibu wa bunge ambao ungeweza kuwa mrefu na wenye madhara zaidi kwa chama cha ANC.

Kiongozi wa ANC, Cyril Ramaphosa anaongoza shinikizo za kumuondoa Zuma katika nafasi yake hiyo ya Urais, na hatimaye kushika pia nafasi hiyo.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW