Michezo

Ancelotti amtumia salamu Mario Gotze

Kocha anayetarajiwa kuchukuwa mikoba ya Pep Guardiola msimu ujao, Carlo Ancelotti amemvunja matumaini ya Mario Gotze kupata namba kwenye kikosi chake msimu ujao.

mariogotze-cropped_1uh0cm43dagbo1pdeu4j9ruufs

Gotze ambaye amekuwa akiwekwa benchi msimu huu na Pep Guardiola na kucheza mechi 20 pekee kwa msimu huu. Hata hivyo chanzo kimoja cha Ujerumani Suddeutsche Zeitung kimedai kuwa Ancelotti amemtaarifu Gotze kwamba ataendelea kuwa mchezaji wa benchi atakapotua kuchukua nafasi ya Guardiola anayetimkia Manchester City mwisho wa msimu.

Gotze amegeuka shujaa wa timu ya taifa Ujerumani baada ya kuifungia bao pekee kwenye fainali ya kombe la dunia dhidi ya timu ya Argentina nchini Brazil mwaka 2014.

Timu ya Liverpool inaonekana kumnyatia kwa ukaribu mchezaji huyo mwenye thamani kati ya paundi milioni 15 hadi 20, amewahi kufundishwa na kocha wa timu hiyo, Jurgen Klopp walipokuwa kwenye timu ya Dortmund.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents