Michezo

Ander Herera athibitisha kuondoka Manchester United, atoa mkono wa kwaheri ‘Nashukuru kwa miaka yote mitano’

Mchezaji wa Manchester United, Ander Herrera amethibitisha kuondoka ndani ya timu hiyo pale mkataba wake utakapofika kikomo mwishoni mwa msimu huu.

Kiungo huyo wa Hispania mwenye umri wa miaka 29  alijiunga na United akitokea kwenye klabu ya Athletic Bilbao mwaka 2014 na kufanikiwa kucheza jumla ya michezo 189 na kufunga mabao 20 huku akitoa pasi za mwisho 25 zilizozalisha magoli.

”Kuna rangi nyekundu, nililijua hilo tangu mara ya kwanza tu kucheza hapa. Nilijiskia fahari pale tu mashabiki walipoamua mimi kuwa sehemu ya historia ya klabu hii. Muda wote nilikuwa nikiiwakilisha, nafahamu inamaanisha nini. Ahsante kwa miaka yote mitano.” Ander Herera amesema hayo kupitia akaunti hiyo.

Herrera alikuwa sehemu ya kikosi cha United kilichotwaa ubingwa wa FA Cup mwaka 2016 ikifuatiwa na ubingwa wa EFL Cup ikifuatiwa na FA Community Shield 2017 pamoja na Europa League 2017 ambapo alitajwa na klabu yake kuwa mchezaji bora wa msimu wa mwaka 2016/17 . Lakini pia mwaka huo huo ametunukiwa tuzo ya Sir Matt Busby Player of the Year na UEFA Europa League Squad of the Season 2017.

Hata hivyo kunako Ligue 1 mabingwa wa ligi hiyo ya Ufaransa PSG wameripotiwa kutaka kumsajili nyota huyo mara baada ya kumalizika kwa mkataba wake na hivyo kujiunga kama mchezaji huru mwishoni mwa mwezi Juni.

Kupitia akaunti yake ya kijamii ya Twitter, Herrera amesema kuwa kuna rangi nyekundu kwenye moyo wake, na aliligundua hilo tangu alipojiunga hapo kwa mara ya kwanza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents