Michezo

Andy Murray athibitisha kushiriki michuano ya Fever-Tree Championships

Mchezaji tennis, Andy Murray amethibitisha kushiriki michuano ya Fever-Tree Championships inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi wiki ijayo kwenye viwanja vya Queen Club huko West Kensington, London.

Bingwa huyo mara mbili wa michuano ya Wimbledon amekuwa nje ya uwanja tangu mwaka jana 2017 baada ya kufanyia upasuaji mwezi Januari.


Cameron Norrie na Murray wakipeana mikono baada ya mazoezi hapo jana siku ya Ijumaa

Murray mwenye umri wa miaka 31, baada ya kufanya mazoezi hapo jana siku ya Ijumaa na Brit Cameron Norrieon amethibitisha kuwa yupo fiti kwa michuano hiyo ya Queen Club Championships ambayo inafanyika kila mwaka inausisha wachezaji tennis wa kiume pekee.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents