Michezo

Andy Murray kuanza na Benoit Paire michuano ya Wimbledon

Mchezaji tennis, Andy Murray amejumuishwa kwenye michuano mikubwa ya Wimbledon baada ya kuwa nje ya uwanja kwa mwaka mmoja kufuatia kusumbiliwa na majeraha aliyopata.

Bingwa huyo mara mbili wa michuano hiyo atakabiliana na Benoit Paire anayeshika nafasi ya 48 kwenye viwango vya ubora wa mchezo huo duniani katika mchezo wake wa raundi ya kwanza.

Murray amecheza michezo mitatu pekee tangu atoke kuuguza majeraha yake aliyopata mwaka jana kwenye michuano hiyo ya Wimbledon ambayo alifanyia upasuaji mwezi Januari.

Baada ya kupata nafasi hiyo ya kushiriki kwenye michuano hiyo mikubwa Murray ameiambia The Times kuwa amejiskia furaha kuwemo kwenye mashindano hayo na kuahidi kushiriki.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents