Burudani ya Michezo Live

Anfield kumekucha, mashabiki waisahau Corona, Liverpool bingwa baada ya miaka 30

Anfield kumekucha, mashabiki waisahau Corona, Liverpool bingwa baada ya miaka 30

Baada ya kulisubiria kombe la Premier League kwa miaka 30, hatimaye klabu ya Liverpool hapo jana walitangazwa kuwa mabingwa wapya.

Liverpool are crowned Premier League champions – live reaction ...

Liverpool imetangaza rasmi kuwa yeye ndiyo bingwa wa ligi kuu England baada ya mpanzani wake kwenye mbio za Ubingwa klabu ya Manchester City kukubali kipigo cha magoli 2-1 dhidi ya Chelsea na hivyobasi kuwathibitisha The Reds kutawazwa sasa kuwa Machampios.

Kikosi cha Jurgen Klopp kilihitaji ushindi katika mchezo mmoja pekee ili kuhalalishwa kuwa mabingwa lakini Chelsea imewasaidia kuutangaza mapema zaidi baada ya kuwafunga Manchester City na hivyo pointi za Majogoo hao wa England kuwa hakuna timu yoyote ambayo itaweza kuzifikia.

Liverpool, Premier League champions: 'A proud supporter of the ...

Hili linakuwa kombe la 19 kwa Liverpool baada ya kufanya hivyo mara ya mwisho msimu wa mwaka 1989-90.

LIVE: Liverpool crowned Premier League Champions — reaction and ...

Licha ya kuwepo kwa janga la virusi vya Corona maelfu ya mashabiki wameshindwa kusalia majumbani ili kuepusha kusambaa kwa ugonjwa huo na badala yake wakajazana Anfield na kuanza kushangilia Ubingwa huo.

LIVERPOOL, ENGLAND - Thursday, June 25, 2020: Liverpool supporters congregate outside the famous Spion Kop at Anfield as they celebrate after their side were crowned Premier League Champions following Manchester City's defeat by Chelsea. The supporters have waited 30 years for this their 19th Championship title. (Pic by David Rawcliffe/Propaganda)

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW