Burudani

Angel Benard: Muimbaji wa gospel wa Tanzania mwenye sauti ya pekee na kipaji kisichoelezeka!

Kuna vipaji vingi vya muziki nchini Tanzania ambavyo bado havijafahamika kwa wengi. Angel Benard ni mmoja wao.

10480595_388713734652934_9052814860540965283_o

Kwa wale wanaohudhuria matamasha ya nyimbo za dini jijini Arusha, jina lake linaweza kuwa si geni na huenda uwezo wake wakawa wanaujua.

Actually mimi nimemfahamu mwanzoni tu mwa mwaka huu. Hii ni kwasababu mimi si msikilizaji sana wa nyimbo za gospel hasa za Tanzania.

Nilimfahamu baada ya kutumiwa link na mtu kwenye akaunti yangu ya Facebook na mtu huyo kunieleza kuwa nifanya mpango wa kumfuatilia msichana huyu.

https://www.youtube.com/watch?v=XxIreY_jfVM

Kwakuwa mara nyingi huwa napokea jumbe nyingi za aina hiyo na nyingi ukizifuatilia unagundua kuwa umepoteza tu muda, sikutilia maanaani. Mara nyingine tena nikapokea ujumbe kutoka mkito.com ambao ulikuwa umeweka wimbo wake, napo sikutilia maanani tena kwakuwa nyimbo za gospel huwa hatuziweki kama ilivyo kwa nyimbo za kawaida.

Kwa mara nyingine tena nikapigiwa simu na mtu kutoka Mkito ambaye aliniomba nimtafute na nimhoji ili kumfahamu zaidi.

Hata hivyo alinirahisishia kazi na kunitumia video ya mahojiano yake ambayo niiliweka kwenye akaunti ya Youtube ya Bongo5. Tena, sikuchukulia ‘serious’ zaidi ya kupost tu habari yenye video hiyo.

Hivi karibuni rapper wa kundi la 909, Kiche Legend alinisikilizisha wimbo wa miaka miwili iliyopita ya rapper aitwaye H.i.M aliyemshirikisha Angel kwenye wimbo wake One Day.

Well, hapo nikagundua kitu tofauti na kujiambia sasa kuwa inabidi nimfuatilie msichana huyu kwakuwa niligundua kuwa sauti yake na uwezo wake si wa kawaida!

Angel ana sauti tamu na ukimpa nafasi akiumbie kwa dakika mbili tu, utagundua kuwa kuimba ni karama aliyopewa na Mungu.

Kama angekuwa anafanya muziki wa dunia, Angel Bernard lingekuwa jina maarufu kwenye redio za Tanzania. Lakini aliamua kuchagua kuimba nyimbo za gospel ambazo hata hivyo zipo kwenye mtindo wa kisasa zaidi ambayo yeye anauita ‘muziki mtamu’.

Angel alianza kuimba akiwa mdogo kabisa japo wimbo wake kwanza aliurekodi mwaka 2006 na ulikuwa wa Bongo Flava.

“Napenda kuimba sweet music,” anasema.

“Mimi ninaamini aina ya muziki ninaoufanya, hauna complication kwahiyo ni kitu rahisi kila mtu kukisikiliza, kukielewa hata akiwa katulia tu anaweza akawa anaisikiliza akaenjoy lakini pia akapata meseji nyuma ya nyimbo ninazoimba.”

Pengine sababu kubwa ya watu kama mimi kushindwa kumfahamu mapema, ni kutokana na changamoto inayomkabili yeye kama muimbaji wa nyimbo za injili kushindwa kuonesha uwezo wake kwenye sehemu tofauti na mikusanyiko ya dini.

“Kuna wakati unaweza ukatamani uimbe sehemu fulani lakini inakulimit sababu ya mentality. Naangalia Kenya, muziki wa gospel unapigwa anytime hata mchana, meseji inaenda kwa watu sahihi kuliko hata ile kuimbiana sisi wenyewe pale kanisani. Mimi naamini ujumbe wangu unatakiwa ufike kwa watu ambao hawaamini kabisa.”

Angel anasema sababu hiyo imefanya nyimbo zake kushindwa kupigwa muda wa mchana hususan kwenye redio za kawaida. “Ni kwasababu umetaja Yesu mle ndani na vitu kama hivyo. ”

Angel alizaliwa June 29, 989, akiwa kama mtoto wa tatu katika familia ya watoto sita: Alfred, Consolatha, yeye, Elizabeth,Anjawe na Lufunyo. Ameanza kuimba akiwa na umri wa miaka 6 katika kanisa la Roman Catholic-Tabata magengeni, akiwa mshirika wa kwaya kuu.

Amesoma Kisutu primary school, Zanaki Secondary school,Mbezi Beach High School na kuhitimu University of
Kipindi chote hicho alikuwa akiimba mchanganyiko wa nyimbo za dini na za kawaida, mpaka alipokuja kukata shauri mwaka 2007 September 26 katika kanisa la Mito ya Baraka.
2008 alirekodi album ya kwanza YOTE YALIKWISHA, 2010 alirekodi nyingine iliyoitwa NITAKUABUDU MILELE. Amekuwa sehemu ya vikundi mbalimbali kama vile Messengers band, Whispers Band, Glorious Celebration (GWT) na Pure Mission.

Kwa sasa ametoa album ya tatu inayoitwa NEW DAY.

Pamoja na kuimba, Angel pia ni mzungumzaji katika maeneo mbalimbali, ni mshauri wa vijana hasa wasichana, ni mwalimu wa sauti na pia mwandishi wa nyimbo.

March 21 mwaka huu, Angel alichumbiwa na Godsave Sakafu na wanatarajia kufunga ndoa mwezi July. Wote wanaishi Arusha.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents