Habari

Angela Merkel ashinda uchaguzi mkuu Ujerumani

Kansela wa Ujerumani , Bi Angela Merkel ameibuka kidedea kwa ushindi katika uchaguzi mkuu nchini humo kwa kuongoza kipindi cha nne.

Merkel kupitia Chama chake cha CDU ameshinda kwa asilimia 32.9 huku wataalamu wengi wa masuala ya kisiasa wakidai kuwa chama chake kimekosa ushawishi ukilingansha na chama cha mrengo wa kulia cha AfD.

Inakadiriwa kuwa chama hicho cha AfD chenye msimamo mkali dhidi ya wahamiaji kitashinda asilimia 13 ya viti bungeni.

Mwenyekiti wa chama cha AfD Frauke Petry, amesema Wajerumani wameshuhudia tetemeko la ardhi kisiasa nchini humo.

Hata hivyo, Merkel ameonesha kutofurahishwa na matokeo ya chama chake ikiwa ni matokeo mengine mabaya kuwahi kutokea katika chama chake katika historia ya Ujerumani, tangu yale ya mwaka 1933 yaliyo muweka madarakani Adolf Hitler.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents