Burudani

Antivirus ipo njiani

Mkongwe wa Bongo Hip Hop, Joseph Mbilinyi ‘Mr. II’ a.k.a ‘Sugu’ amewakusanya masela kibao kunako anga za muziki huu na kuanzisha very active project inayokwenda kwa jina la ANTIVIRUS. “Project hiyo inahusu mapinduzi, inanyoosha ukweli kwa vipimo vyake, inawagonga fatuma wezi wote waliohusika kuihujumu Bongo Fleva na inatangaza vita kwa yeyote mwenye shida ya ubaya dhidi ya wanamuziki wataka haki” alisema Sugu.

 

Kwa mujibu wa Sugu, Antivirus ni project ya mashambulizi mwanzo mwisho, itafanya kazi kwa mtindo wa mixtapes, yaani kurekodi nyimbo kwenye instruments maarufu za kiwanja, halafu ngoma zinawekwa pamoja halafu zinagawiwa bure kwa Watanzania. “Kila msanii ataimba topic yake kuhusu Antivirus, yaani atagonga jiwe lake kwa kutaja majina wahusika wa unyonyaji wa muziki wetu.

Watu ambao wanaua muziki. Tunagawa bure ili kutaka ujumbe ufike kwa Watanzania,” ……“Ni bure na kazi yote itasajiliwa COSOTA kwamba haiuzwi. Mtu anaruhusiwa kutoa nakala na kumpa mwenzake. Itatoka Antivirus part I mpaka kumi kisha itakuja Antivirus Vol II. Wasanii wapo wengi na toleo la kwanza litakuwa na nyimbo 16.”

Baadhi ya Ma-Lijendari watakaokuwemo kwenye project hiyo ni Godfrey Tumaini ‘Dudubaya’, Suleiman Msindi ‘Afande Sele’, G Solo na wengine kibaoooooooo.

Project hiyo inasimamiwa na Fredy Maliki ‘Mgosi Mkoloni’, Danny Msimamo na Dotto Maujanja kutoka crew ya mapacha.

Alisema Sugu.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents