Michezo

Antonio Conte hataki kuniona Chelsea -Diego Costa

Mshambuliaji wa klabu ya Chelsea, Diego Costa amesema kuwa  Meneja wa wake, Antonio Conte  amemuambia hana mipango naye ya muda mrefu ndani ya kikosi hiko.

Mshambuliaji wa klabu ya Chelsea, Diego Costa akipiga mpira golini mwa Arsenal

Mchezaji huyo (28) amefunga jumla ya magoli 20 katika michezo yake 35 aliyocheza katika ligi kuu ya Uingereza katika msimu uliomalizika hivi karibuni na kuisaidiaThe Blues kutwaa taji la ligi – Costa amejitokeza na kutangaza kutaka kuondoka Stamford Bridge.

Meneja wa Chelsea, Antonio Conte

“Mimi ni mchezaji wa Chelsea , lakini wao hawanihitaji. Antonio Conte aliniambia kupitia ujumbe mfupi wa maandishi ’ message’  niachane na Chelsea na kamwe hato nijumuisha katika kikosi cha msimu ujao,” amesema  Costa baada ya kumalizika kwa mchezo nwa kirafiki kati ya Hispania dhidi ya Colombia.

Mshambuliaji wa klabu ya Chelsea, Diego Costa akikumbatiwa na meneja, Antonio Conte

Mchezaji huyo ameongeza kwa kusema, “Mahusiano yangu na kocha  yamekuwa si mazuri katika msimu huu. Niaibu, tayari nimesha usambaza ujumbe huo kwa watu wa Chelsea waamue wenyewe.

Ujumbe ambao     Conte alimtumia Diego unasomeka, “Unapaswa kutafuta timu nyingine.” Costa alijiunga na Chelsea akitokea katika klabu ya Atletico Madrid  kwa dau la paundi milioni 32 mwaka  2014.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents