Michezo

Antonio Valencia na Ander Herera wang’ara kwenye tuzo za mwaka (+Picha)

By  | 

Klabu ya Manchester United jana imefanya hafla ya kukabidhi tuzo kwa wachezaji wake waliofanya vizuri kwa msimu huu unaomalizikia,Tuzo ambazo  Antonio Valencia ameibuka na kuwa mchezaji bora wa mwaka akiwapiga bao nyota wengine akiwemo Zlatan Ibrahimovic.

Mchezaji bora wa Mwaka wa Klabu ya Man United ‘Antonio Valencia’ akiwa na tuzo yake

Antonio Valencia amewapiga bao wachezaji wenzake wa Klabu hiyo akina Zlatan Ibrahimovic,Pogba na Rashford kwenye kinyang’anyiro cha mchezaji bora wa Mwaka huku tuzo ya Goli bora la msimu tuzo ikienda kwa Henrikh Mkhitaryan huku mchwezaji kinda wa klabu hiyo tuzo imeenda kwa Angel Gomes.

Henrikh Mkhitaryan akichukua tuzo ya goli bora la Msimu

Wengine walioshinda tuzo ni Ander Herera tuzo ya mchezaji bora wa Mwaka aliyechaguliwa na mashabiki na Kinda Angel Gomes ameshinda tuzo ya mchezaji kinda wa mwaka.

Ander Herera akiwa na Tuzo yake kushoto ni Goli kipa wa Man United De Gea

Angel Gomes

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments