Burudani

Antu Mandoza ageuka kungwi mtandaoni, awafunda wanawake wanaopenda wanaume wenye vitu vya thamani

Muigizaji na Mjasiriamali, Mrembo Antu Mandoza amewafunda wasichana wenzake kuwa waache tabia ya kumpenda mwanaume kwa sababu ya vitu anavyomiliki.

Antu akitoa darasa hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram, ameandika kuwa wanawake wanatakiwa watambue kuwa mali za mwanaume ni zake, huku akiwataka wawe makini sana la sivyo wataishia kuchezewa.

Kina dada, mabinti, wasichana Hebu tuskilizane kwenye hili.
Tuache tabia ya kutengeneza hisia za kimapenzi kwa wanaume kutokana na kitu alichonacho au ulichomuona nacho kwa mara ya kwanza kama vile umeambiwa anavokutongoza Ndio kaweka ahadi/contract ya kukupatia mali zake 🤣😂.
Karne hii bado kuna mtu anadanganyika na Gari mtu anayoendesha? Ni Gari yake sio Yako , oh ana kiwanda ni chake sio chako, ana nyumba 7 ni zake sio zako ana cheo ni chake sio chako, Tusijimilikishe kimawazo , atakuvua nguo Afu humuoni ubaki Una Laani😂.
Chochote kile Until you benefit in reality , until he buys or give it to you kwa documents OG usijihakikishie umiliki wala kujirahisisha watakutumia wakimbie dada.
I thought of writing this just a few minutes ago kwa maskio yangu i heard kijana akiongea na simu akimuazima gari rafiki yake akamrubunie msichana “ Oya mwanangu nleetee basi hio Benz hapa shoppers nikang’oe mtoto naskia chizi magari yule dem”
Aisee nikajiskia vibaya 😔😣,hata aje na helkopa it’s not yours mjaji kwa maneno na hisia zako kwake sio kisa ana range, utadanganyika akishapata anachotaka atarudi zake kwenye Tz 11 Au Corolla yake we ubaki unaota Au unalia , tusiwe na expectation kubwa na kupigia hesabu Mfuko wa mtu kabla hujamjua vizuri , watu wasanii bwana 😅. Tafuta chako , cha mtu Mavi , wafundisheni na watoto wenu hivo.
I’m that honest and real . Jumapili njema.

Antu Mandoza ni moja ya wanawake wajasiriamali wenye umri mdogo Tanzania na alishawahi kuigiza filamu kadhaa ikiwemo ile ya Kiumeni.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents