Uncategorized

Anyolewa nywele na mumewe kwa kukataa kucheza dansi

Mwanamke mmoja raia wa Pakistani amemshutumu mume wake hadharani kwa kumpiga na kumnyoa nywele baada ya kukataa kucheza mbele ya mwanaume huyo akiwa rafiki zake, Kesi ambayo imeleta maswali mengi kuhusu usalama wa wanawake nchini humo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Asma Aziz, kutoka jimbo la Lahore, alisababisha kuzungumzwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari duniani baada ya kusambaza video kwenye mitandao ya kijamii akionyesha kichwa chake kilichonyolewa na uso wenye alama zilizotokana na vipigo.

Mume wake, Mian Faisal, na msaidizi wake wote wanashikiliwa na polisi. Bwana Faisal amekana kumtesa mkewe.

Hata hivyo, tukio hilo limeamsha hisia kali na kutolewa wito kuwa hatua zaidi zichukuliwe ili kukomesha unyanyasaji.

Katika ukurasa wake wa Twitter, Shirika la Amnesty International limesema mabadiliko ni lazima.

Katika video iliyowekwa tarehe 26 mwezi Machi, Bi Aziz alidai kuwa siku mbili zilizopita aliteswa baada ya kukataa kucheza muziki mbele ya marafiki wa muewe ambao walifika nyumbani kwao.

”Alinivua nguo mbele ya wafanyakazi wake. Wafanyakazi walinishika wakati akininyoa nywele na kuzichoma. Nguo zangu zilijaa damu. Nilikua nimefungwa, akatishia kunining’iniza nikiwa mtupu,” alieleza.

Alisema alipokwenda polisi kufungua mashtaka polisi hawakuonyesha kujali.Lakini polisi walijiteteta kuwa mara tu baada ya Bi Aziz kuripoti askari waliondoka kuelekea kwenye makazi ya mlalamikaji lakini waliikuta nyumba imefungwa na hawakuruhusiwa na mamlaka ya ulinzi wa makazi kuingia eneo hilo

Polisi walichukua hatua baada ya video hiyo kuonwa na naibu waziri wa mambo ya ndani Sheheryar Afridi, ambaye aliamuru mwanamke huyo asikilizwe.

Bwana Faisal na wafanyakazi wake walikamatwa siku iliyofuata. Ripoti ya awali ya daktari imeonyesha majeraha, uvimbe na wekundu kwenye mikono ya Bi Aziz na kuzunguka jicho lake la kushoto.

Mawakili wa Bi Aziz wamesema kesi hiyo iko chini ya sheria ya kupambana na ugaidi badala ya uhalifu wa kawaida.

Mawakili wamesema kesi hiyo imeleta hali ya mshangao na hofu kwenye jamii.

Bwana Faisal aliwaambia polisi juma lililopita kuwa mke wake alianza kukata nywele akishawishiwa na madawa na kwamba yeye pia alikula madawa, ambayo yalimsaidia kumaliza kazi yake.

Kesi hiyo ilisababisha mjadala mkali kwenye mitandao ya kijamiii, wengi wakieleza hasira zao kuhusu unyanyasaji nchini Pakistan.

Mcheza filamu na muimbaji Sanam Saeed alikua mmoja kati ya waliozungumzia madhila ya Bi Aziz.

Haki za wanawake imekua hoja ya miaka mingi sana kwa muda sasa.

Umoja wa Mataifa umeiweka Pakistani kwenye orodha kuwa ya 147 kati ya nchi 188 zenye rekodi mbaya kuhusu masuala ya afya ya wanawake, elimu, siasa na uchumi.

Unyanyaaji dhidi ya wanawake na wasichana bado ni tatizo kubwa .Wanaharakati wanasema takwimu hazionyeshi ukubwa wa tatizo.Matukio mengi hayajaripotiwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents