Habari

Apigwa miaka 30 jela kwa kumpa mimba dada yake

Mwanaume mmoja aliyejulikana kwa jina la Charles Abel (24) Mkazi wa kijiji cha Usagara Mkoani Mwanza,  amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela, kwa makosa mawili ya kubaka na kumpa mimba mwanafunzi wa darasa la saba ambaye ni mtoto wa baba yake mkubwa.

Image result for ampa mimba

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Misungwi, Erick Marley akisoma hukumu hiyo juzi alisema amechukua maamuzi hayo baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka.

Akitoa ushahidi mahakamani hapo, Mwanafunzi huyo aliiambia mahakama kwamba mnamo Juni 6 saa 1:30 usiku akiwa chumbani kwake aliingiliwa na kubakwa na kaka yake (Charles Abel) ambaye ni mtoto wa baba yake mkubwa.

Mshtakiwa akijijitetea mahakamani hapo, aliomba kupunguziwa adhabu akidai kuwa hawezi kufanya mapenzi na dada yake na kwamba ametengenezewa kesi hiyo .

Hakimu Marley alisema Mahakama inamhukumu mshtakiwa kwa kosa la kwanza la ubakaji kifungo miaka 30 jela na kwamba, shtaka la pili la kumpa mimba mwanafunzi atatumikia miaka 30 jela, huku akielea kuwa sababu adhabu zote zinakwenda pamoja atatumikia miaka 30 tu badala ya miaka 60.

Chanzo:http://www.mwananchi.co.tz/habari/Aliyempa-mimba-dada-yake-miaka-30-jela/1597578-4833456-4447qb/index.html

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents