Technology

Apple imekuwa kampuni ya kwanza duniani kuwa na thamani ya trilioni 1

Kampuni ya simu na kompyuta Apple imekuwa ni kampuni ya umma ya kwanza duniani kuwa na thamani ya dola trilioni moja $1 trillion.

Bwana Jobs, ambae alifariki dunia mwaka 2011 na kurithiwa na Mkurugenzi Mkuu Tim Cook, alisimamia maendeleo ya iPhone, ambayo ilibadili kabisa kipato cha Apple.

Thamani ya soko la watengezaji wa iPhone imefikia kiwango hicho mjini in New York Alhamisi na hisa zake zilifikia rekodi mpya ya $207.39.

Hisa zake zimekuwa zikipanda tangu Jumanne wakati kampuni hiyo iliporipoti kupata matokeo mazuri kuliko ilivyotarajiwa katika kipindi cha miezi mitatu kuelekea mwezi Juni.

Apple iliipiku kampuni shindani za Silicon Valley kama vile Amazon na Microsoft na kuweza kufikia hadi thamani ya dola trilioni $1.

Tangu iPhone filipowekwa sokoni kwa mara ya kwanza mwaka 2007, hisa za Apple zimekuwa zikipanda kwa 1,100% a na kuongezeka takriban mara tatu katika kipindi cha mwaka uliopita.

Ongezeko hilo ni bora zaidi kwa kiwango cha 50,000% – tangu kampuni hiyo iliposajiliwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 1980.

Kiwango hicho kimepita ongezeko la 2,000% la kiwango cha S&P 500 katika kipindi sawia.

Apple ilianzishwa na muasisi mwenza wa kituo cha kutengeneza magari Steve Jobs mnamo mwaka 1976 na mwanzo ilifahamika zaidi kama kutengeneza komyuta za kibinafsia aina ya Mac kabla ya soko lake la smartphone kufungua njia ya uchumi wa app.

Mnamo mwaka 2006 kampuni hiyo ilikuwa na mauzo ya chini ya $20bn na kutangaza faida ya takriban $2bn.

Mwaka jana mauzo yake yalipanda hadi kufikia $229bn, na faida ya $48.4bn, na kuifanya kuwa kampuni yenye faida kubwa zaidi miongoni mwa makampuni ya Marekani.

PetroChina iliwahi kuwa na thamani ya trilioni $1.1 kwa kipindi kifupi baada ya kuendesha shughuli zake mjini Shanghai in 2007, licha ya kwamba nyingi kati ya hisa zake zilishikiliwa na serikali ya Uchina, kwa sasa inathamani ya takriban dola bilioni 220 ($220bn).

Licha ya kupata thamani ya trilioni $1 , wachanganuzi wa masuala ya kiuchumi bado hawaoni hisa za Apple kama ghali ikizingatiwa kwamba wanaendesha biashara ya takribani mara 15 ya faida iliyotarajiwa, ikilinganishwa na ile ya Amazon ambayo ni mara 82 na mara 25 ya Microsoft.

Hali kadhalika kuongezeka kwa hisa za Apple katika miezi ya hivi karibuni ulikuwa ni uamuzi wa kampuni hiyo wa kutenga dola bilioni 100 ( $100bn) kununua hisa.
Source: BBC na The Guardian.

Related Articles

11 Comments

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents