Technology

Apple wahaha kufuatia ripoti za iPhone kushika moto

Kampuni ya Apple inahaha baada ya simu za iPhone kudaiwa kuanza kushika moto.

the-apple-iphone7-and-airpods-are-displayed-during-an-apple-media-event-in-san-francisco

Kampuni hiyo imedai sababu hiyo imetokana na madhara ya nje ya simu ambayo yameripotiwa kusababisha simu kulipuka au kushika moto nchini China.

Imesisitiza kuwa simu hizo hazina tatizo lolote.

Kampuni inayofuatilia wateja ya Shanghai Ijumaa iliyopita ilidai kuwa imepokea ripoti nane hivi karibuni za iPhones kushika moto wakati zikitumika au zikiwa kwenye chaji.

Ripoti za kulipuka kwa simu hizo zimekuja miezi michache tu baada ya Samsung kupata hasara kubwa kutokana na kulipuka kwa simu za Galaxy Note 7 kiasi cha kusitisha kuzitengeneza.

Apple imesisitiza kuwa tatizo hilo haliwezi kuwa kubwa kama simu za Samsung.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents