Habari

Ardo King atua Bongo toka Chicago, kuanzisha kampuni kubwa itakayokuwa na studio ya muziki, video,filamu, sound system ya kimataifa na kusimamia wasanii

Rapper wa Tanzania aishiye Chicago nchini Marekani, Ardo King, amerejea nchini kwa kishindo akiwa na malengo makubwa katika muziki wa Tanzania. Haya ni maelezo aliyoitumia Bongo5 baada ya kutua nchini:

417777_529821137069129_439800436_n
Ebwana nimetua bongo nina siku kadhaa sasa nikiwa likizo. Nimeachia kazi yangu mpya ya kiswahili kutoka Vitu mbali mbali vya Redio hapa nchini inayotambulika kama “Mwanahiphop wa kweli” ambayo ni utambulisho wangu mpya wa kurudi katika game la nyumbani Baada ya kukaa kimya kwa muda nikiwa ninajipanga upya kuikabili game hii ya sasa ambayo ina mabadiliko makubwa tofauti na ya zamani.

[soundcloud url=”http://api.soundcloud.com/tracks/96816025″ params=”” width=” 100%” height=”166″ iframe=”true” /]

Licha ya kuamua kufanya muziki wangu nchini Marekani, nilipata fursa ya kuutathmini na kuuchunguza muziki na uandishi wa muziki wa hip hop toka nyumbani kwa Mara kadhaa ndipo nikaona kuwa bado ninayo nafasi kubwa ya kurudisha au kuweka heshima katika ulimwengu ya kufokafoka na uandishi wa mashahiri uliokomaa zaidi.

Ninatarajia kuanza maandalizi ya video ambayo pia ni njia moja ya kuitambuliza kampuni ya Legendary Music Entertainment Inc nchini Tanzania, chini ya Legendary music label, itakayo miliki Recording studio kubwa na ya kisasa zaidi, studio ya video na films productions ambayo ndio inafanya video yangu, music systems na DJ machines, Stage kubwa za hadhi ya juu ya kimataifa inayofunguliwa na kufungwa kitaalamu kwa ajili ya matamasha makubwa sana ndani wa Fiesta au Kili Music Awards pia vifaa vya kufanyia P.A.

Kampuni hii itakuwa ina miliki wasanii na kufanya production hadi distribution ili kuinua wasanii na industry nzima. Project hii ni matunda ya kuchanga mawazo yangu na Producer Amarido ambaye maskani yake ni nchini Japan, aliyekuwa akizuru jijini Chicago kwa mafunzo ya kozi fupi za sound engineering na music production ili kuongeza ujuzi zaidi.

Baada ya kufikia makubaliano haya ya uwekezaji hapa nchini, tuliweza kufanya kazi hii huku yeye akiwa ndiye producer na pia tukachukua vacation ya muda na kwa sasa Wote tupo hapa nchini kwa ajili ya kutekeleza haya yote.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents