Michezo

Argentina waanza kwa kichapo Copa Amerika, Maradona amchana Messi ‘Hafai kuwa kiongozi, Natamani Ronaldo angekuwa Muargentina’

Jana usiku michuano ya Cpa America imeendelea ambapo kulikuwa na mchezo wa kukata na shoka kati ya Argentina dhidi ya Colombia, ambapo Argentina walikubali kichapo cha goli 2-0.

Lionel Messi

Mchezo huo uliokuwa wa kusisimua, Uliibua hisia tofauti tofauti kwa magwiji wa soka duniani akiwemo Diego Almando Maradona ambaye yeye alimchana Kapteni wa timu ya taifa ya Argentina mbaye pia ni Kapteni wa klabu ya Barcelona, Lionel Messi kuwa hafai kuwa kiongozi wa timu hiyo.

Akiomtolea mfano hasimu wake na Messi, Cristiano Ronaldo amesema anavyomuangalia Ronaldo anavyopambana na timu yake ya Taifa (Ureno) utagundua kuwa ni mtu mwenye sifa za kuwa kiongozi anawapa wenzake ari ndani na nje ya uwanja tofauti na Messi.

Ronaldo atabaki kuwa ni kiongozi na mchezaji wa mfano, Angalia anavyopambana akiwa uwanjani na hata anavyokuwa na wenzake, yule ni kiongozi. Messi hafai kuwa kiongozi na hana haiba hiyo kwa wachezaji wenzake wa Argentina. Natumaini siku moja Ronaldo atakuja kuichezea Argentina.“amesema Maradona kwenye mahojiano yake na ESPN muda mchache baada ya mchezo huo.

Kwa matokeo hayo ya mchezo wa kwanza, Colombia wanaongoza kundi B huku Argentina wakishika mkia, timu nyingine kwenye kundi hilo ni Paraguay na Qatar.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents