Michezo

Argentina yabanwa mbavu na Iceland, Lionel Messi akosa penati

Timu ya taifa ya Argentina imeshindwa kutamba mbele ya Iceland baada ya kulazimishwa sare ya bao 1 – 1 kwenye mchezo wa kombe la dunia huko Urusi licha ya kuwa na wachezaji wenye majina makubwa ndani ya kikosi chake.

Dakika ya 19 ya kipindi cha kwanza, Sergio Aguero alianza kuifungia Argentina bao la kuongoza kabla ya kusawazishwa na mchezaji wa Iceland, Finnbogason dakika ya 23.

Katika hali isiyotarajiwa mshambuliaji wa timu ya taifa ya Argentina na klabu ya Barcelona, Lionel Messi amekosa mkwaju wa penati dakika ya 64 ya mchezo jambo ambalo limewashangaza wengi.

Kikosi cha Argentina: Halldorsson, Saevarsson, Sigurdsson, Arnason, Magnusson, Gudmundsson, Bjarnason, Gunnarsson, Hallfredsson, Sigurdsson, Finnbogason

Waliyokuwa benchi: Schram, Runarsson, Ingason, Eyjolfsson, Skulason, Fridjonsson, Gudmundsson, Skulason, Traustason, Sigurdarson, Gislason, Bodvarsson

Kikosi cha Iceland: Caballero, Tagliafico, Rojo, Otamendi, Salvio, Biglia, Di Maria, Meza, Mascherano, Messi, Aguero

Waliyokuwa benchi: Guzman, Armani, Mercado, Ansaldi, Fazio, Banega, Acuna, Perez, Lo Celso, Higuain, Dybala, Pavon

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents