Burudani

Ariana Grande athibitisha kufanya show nyingine mjini Manchester

Baada ya show ya Ariana Grande ya Jumatatu Mei 22 mjini Manchester, Uingereza kuingia dosari kwa kusababisha vifo vya watu 22 na wengine zaidi ya 50 kujeruhiwa kutokana na mlipuko, msanii huyo amepanga kufanya show kubwa kwa mashabiki wake.

Muimbaji huyo wa muziki wa Pop kutoka Marekani, ameahidi kurudi tena katika mji huo kwaajili ya kuwafariji na kuwatia moyo mashabiki zake kwa kufurahia pamoja huku akitarajiwa kufanya show nyingine. Hilo amethibitisha Ariana mwenyewe kutokana na barua yake aliyoiweka katika mtandao wa Instagram.

Hata hivyo mtandao wa TMZ, uliripoti kuwa show hiyo ya Grande ya Uingereza inatafanyika Juni 5 ya mwaka huu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents