Burudani

Ariena Grande alivyowatembelea majeruhi wa mlipuko Manchester

Ariana Grande amewatembelea mashabiki wake waliokuwa hospitali ambao walilazwa kutokana na tukio la mlipuko uliolotokea Mei 22 mjini Manchester katika show ya ziara yake ya “Dangerous Woman World” na kusababisha vifo vya watu 22 na wengine zaidi ya 50 kujeruhiwa.

Muimbaji huyo wa muziki wa Pop amefanya jambo hilo ikiwa ni siku moja imebakia kabla ya kufanya show nyingine katika mji huo iliyopewa jina la “One Love Manchester.”

Katika show hiyo inayotarajiwa kufanyika Jumapili ya Juni 5 katika uwanja wa Emirates Old Trafford Cricket Ground wenye uwezo wa kuchukuwa watu takriban 50,000, Ariena atawasha moto akiwa pamoja na wasanii wengine kama Justin Bieber, Coldplay, Katy Perry, Miley Cyrus, Pharrell, Usher, na Niall Horan.

Show hiyo itaonyeshwa moja kwa moja kupitia kituo cha runinga cha ABC na vingine. The Universal Music Group ambao wanamsimamia msanii huyo wanatarajia kukusanya kiasi cha dola 500,000 kwa ajili ya kuchangia katika mfuko uiliopewa jina la “We Love Manchester Emergency Fund.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents