Michezo

Arsenal chupuchupu, Wenger atupa lawama kwa muamuzi

Klabu ya Arsenal hapo jana imetoka sare ya mabao 2-2 mbele ya Chelsea katika mchezo wa ligi kuu nchini Uingereza maarufu kama London derby.

Meneja Arsene Wenger amemshushia lawama muamuzi wa mchezo huo, Anthony Taylor kwa kuipatia Chelsea penati ambayo anaamini haikustaili na kuifanya timu hiyo kusawazisha bao kupitia kwa Eden Hazard dakika ya 67.

The Gunners ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa mchezaji wake Jack Wilsher dakika ya 63 lakini Eden Hazard akaisawazishia Chelsea dakika nne baadae kisha Marcos Alonso akiandikia The Blues bao la kuongoza dakika ya 84 kisha Hector Bellerin akaibuka shujaa wa mchezo baada ya kuisawazishia Arsenal bao la pili dakika za nyongeza na kuufanya  kumalizika kwa sare ya 2-2.

Mchezaji,  Marcos Alonso akiiandikia The Blues bao la kuongoza dakika ya 84

Kikosi cha Arsenal Cech (7), Holding (6), Mustafi (6), Chambers (5), Bellerin (7), Xhaka (6), Wilshere (7), Maitland-Niles (6), Ozil (8), Sanchez (7), Lacazette (6).

Waliyokuwa benchi: Walcott (5), Welbeck (5).

Chelsea: Courtois (8), Cahill (6), Christensen (6), Azpilicueta (6), Moses (5), Kante (6), Bakayoko (5), Alonso (7), Fabregas (6), Hazard (8), Morata (6).

Waliyokuwa benchi: Drinkwater (5), Zappacosta (6), Willian (5).

Eden HazardEden HazardEden Hazard

Mchezaji bora wa mchezo huo ni Eden Hazard.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents