Michezo

Arsenal inaweza kuchukua Ubingwa wa EPL – Granit Xhaka

 

Kiungo wa klabu ya Arsenal, Granit Xhaka amesema kuwa timu yake inaweza kuwapiku viongozi wa ligi kuu nchini Uingereza Manchester City na kuwania ubingwa huo wa EPL.

Kiungo wa klabu ya Arsenal, Granit Xhaka

Arsenal ambayo imechomoza na ushindi wa mabao 2-0 dhidi Tottenham Hotspur siku ya Jumamosi imepanda hadi nafasi ya sita katika msimamo wa ligi kwakuwa na jumla ya pointi 22 ikiachwa nyuma kwa alama 12 na City huku Xhaka akiamini timu hiyo inaweza kurejea katika ushindani wa kuwania taji la EPL.

“Nadhani katika mchezo wa mpira wa miguu kilakitu kinawezekana,” Xhaka alikiambia chombo cha habari cha Sky Sports.

Granit Xhaka ameongeza “Manchester City kwa wakati huu inafanya vizuri na baadhi ya timu nyingine zinazidi kupoteza pointi jambo ambalo halikutokea kabla.”

“Mimi ni mwanadamu ambaye nafikiria lakini nina ndoto pia katika soka kilakitu sikuzote hutokea na huwekana .”

City imeweza kumiliki ushindani na kufanya vizuri hali iliyopelekea kufunga jumla ya mabao 40 katika mashindano yote na kuongoza kwa alama nane dhidi ya Manchester United inayoshika nafasi ya pili lakini Xhaka anaamini kikosi cha Pep Guardiola kitafika kipindi kitashuka na Arsenal itachukua hatamu ya uongozi wa ligi.

Arsenal inatarajia kucheza na FC Cologne katika michuano ya Europa League siku ya Alhamisi kisha kukutana na Burnley siku ya Jumapili katika ligi ya Uingereza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents