Moto Hauzimwi

Arsenal kama kawaida yao ligi kuu, Liverpool kazi kazi

Usiku wa kuamkia leo (Jumatano) michezo minne ya ligi kuu ya Uingereza imeendelea kuchezwa. Arsenal ambao walikaribishwa na Swansea City katika uwanja wa Liberty na walifungwa kwa magoli 3-1.

Magoli ya Swansea yalifungwa na Samuel Clucas kwenye dakika ya 34 na 86 na la tatu lilifunywa na Jordan Ayew dakika ya 61. Goli la kufutia machozi la Arsenal lilifungwa na Nacho Monreal dakika ya 33.

Wakati huo huo katika mechi nyingine, Liverpool ambao siku ya Jumamosi ya January 27 walitolewa katika raundi ya nne ya kombe la FA, walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Huddersfield.

Magoli ya Liverpool yalifungwa na wachezaji wao Emre Can dakika ya 26, Roberto Firmino kwenye dakika 45 na Mohamed Salah dakika ya 78.

Katika mechi nyingine West Ham United walitoka sare ya kufungana bao 1-1 na Crystal Palace. Mechi nyingine zinatarajiwa kuchezwa leo (Jumatano) huku mchezo ambao unasubiriwa kwa hamu kubwa ni kati ya Manchester United ambao watakuwa ugenini kucheza dhidi ya Tottenham Hotspurs.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW