Michezo

Arsenal yaanza kurejesha paundi milioni 53 za Lacazette

Mchezaji mpya wa klabu ya Arsenal aliyesajiliwa akitokea, Lyon ya Ufaransa, Alexandre Lacazette ameanza kuirudishia faida timu yake baada ya hapo jana usiku kuifungia mabao muhimu katika mchezo wao wa Ligi Kuu nchini Uingereza dhidi ya West Bromwich Albion.

Lacazette ambaye ni mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ufaransa alikuwa mwiba mkali hapo jana usiku mbele ya West Bromwich Albion baada ya kuifungia The Ganners jumla ya mabao 2 -0.

Mchezaji huyo aliyekuwa akikipiga League One ya nchini Ufaransa mpaka sasa amevunja rekodi ya mmchezaji Brian Marwood iliyowekwa mwaka 1988 ya kufunga katika michezo mitatu ya mwanzo ya Ligi ya Kuu ya Uingereza.

Kwa ushindi huo wa hapo jana usiku unaifanya The Ganners kusalia katika nafasi ya saba ya msimamo wa wa Ligi Kuu ya Uingereza kwakuwa na pointi 10.

Msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents