Michezo

Arsenal yafanikiwa kumnasa, Willian 

Arsenal imemsajili kiungo wa kati wa Brazil, Willian kwa mkataba wa miaka mitatu baada ya mkataba wa mchezaji huyo, 32, kukamilika.

Welcome Willian! | Brazil forward joins Arsenal | News | Arsenal.com

The Blues ilitoa ofa yake mpya kwa mchezaji huyo lakini haikuwa tayari kufikia kile ambacho the Gunners imempa.

“Naamini ni mchezaji ambaye kweli anaweza kutufanyia mabadiliko makubwa,” amesema kocha wa Arsenal Mikel Arteta.

“Tulikuwa tumedhamiria kabisa kuimarisha upande wa kushambulia wa kuingo wa kati na nafasi ya winga.”

Willian alishiriki michezo 339 katika klabu ya Chelsea baada ya kusajiliwa kutoka klabu ya Anzhi Makhachkala ya Urusi kwa pauni milioni 30 mwaka 2013.

“Ni mchezaji ambaye tunaweza kumbadilisha badilisha, Anaweza kucheza nafasi tatu au nne tofauti. Nimefurahishwa sana na mazungumzo yangu nae na jinsi alivyokuwa anataka kujiunga nasi.”Arteta ameongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents