Michezo

Arsenal yaingia 16 bora, matokeo ya mechi za UEFA Dec 9

Michezo ya hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya iliendelea tena usiku wa December 9 kwa mechi nane baada ya makundi ya E, F, G na H, michezo hiyo ilichezwa wakati timu 10 kati ya 32 zikiwa zimeshajihakikishia nafasi ya kwenda hatua ya 16 bora hivyo nafasi 6 pekee ndio zilikuwa zinawaniwa.

2F37676500000578-0-image-a-46_1449694670245

2F379FD000000578-0-image-a-69_1449695516399

Klabu ya Arsenal ambayo ilikuwa nafasi ya tatu katika msimamo wa Kundi F, nafasi yake ya kuendelea hatua ya 16 bora ilikuwa mikononi mwake yenyewe, ilifanikiwa kuifunga Olympiakos ya Ugiriki magoli 3-0 magoli yote yalifungwa na
mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa Oliver Giroud, staa huyo alifanikiwa kuipeleka Arsenal hatua ya 16 bora alianza kufunga goli la kwanza dakika ya 29, kipindi cha pili akamalizia kwa kupachika magoli mawili dakika ya 49 na dakika ya 67 kwa mkwaju wa penati baada ya beki wa Olympiakos kushika mpira katika eneo la 18.

Hizi ndo timu zilizo fanikiwa kufuzu hatua ya 16: Real Madrid, PSG, VfL Wolfsburg, PSV Eindhoven, Atletico Madrid, Benfica, Man City, Juventus, FC Barcelona, Roma, FC Bayern Munich, Arsenal, Chelsea, Dynamo Kiev, Zenit St P,KAA Gent.

Matokeo ya mechi nyingine za UEFA za December 9

Kundi E

Bayer Leverkusen 1 – 1 FC Barcelona
Roma 0 – 0 BATE Borisov

Kundi F

Dinamo Zagreb 0 – 2 Bayern Munich
Olympiacos 0 – 3 Arsenal

Kundi G

Chelsea 2 – 0 FC Porto
Dynamo Kyiv 1 – 0 Maccabi Tel Aviv

Kundi H

Gent 2 – 1 Zenit St. Petersburg
Valencia 0 – 2 Lyon

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents