Michezo

Arsenal yamfungulia milango Ramsey, aambiwa yupo huru kuondoka Man United, Juve na Bayern za haha saini yake

Klabu ya Arsenal imemfungulia milango nyota wake, Aaron Ramsey kuwa yupo huru kuondoka mwishoni mwa msimu huu na haina mpango wa kumuongezea mkataba mpya.

Ramsey amesikika kwenye mahojiano yake na gazeti moja wiki iliyopita kuwa hajapata taarifa yoyote kuhusiana na kuongezewa mkataba wake ambao unaelekea ukingoni mwa msimu huu.

Arsenal haiyamini kuwa lipo soko la usajili wa mwezi Januari ambalo litaiwezesha kuingiza fedha hivyo Ramsey ataondoka akiwa mchezaji huru.

Hata hivyo klabu za Juventus, Bayern Munich, Manchester United na Chelsea zinaangazia kwa ukaribu kuona kama zitafanikiwa kunasa saini ya mchezaji huyu.

Ramsey amejiunga na the Gunners mwaka 2008 akitokea kwenye klabu ya Cardiff na kufanikiwa kucheza jumla ya michezo 343 wakati msimu huu akiwa ameshiriki kucheza mechi 12 kwenye mashindano yote.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents