Michezo

Arsenal yasajili beki kisiki wa Bosnia

Klabu ya Arsenal ya nchini Uingereza imetangaza kumchukua beki wa kushoto wa timu ya taifa ya Bosnia, Sead Kolasina.

Mchezaji wa klabu ya Schalke 04 ya nchini Ujerumani, Sead Kolasina.

Beki huyo aliye kuwa akikipiga katika klabu ya Schalke 04 ya nchini Ujerumani anatarajiwa kuanza majukumu yake majira ya joto msimu ujao.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23, ambaye huchezea timu ya taifa ya Bosnia-Herzegovina, amejiunga na Arsenal bila kulipiwa pesa yoyote kwenye klabu yake kwa kua mkataba wake unamalizika msimu huu ndani ya klabu hiyo .

Mchezaji huyo atakuwa rasmi mchezaji wa Arsenal mwezi Julai baada ya dirisha la usajili litakapo funguliwa.

Mchezaji wa klabu ya Schalke 04 ya nchini Ujerumani, Sead Kolasina.

Arsenal imesema beki huyo atajiunga na klabu kwa ajili ya kujiweka sawa kabla ya msimu wa ligi kuanza
Schalke, wamethibitisha kwamba beki huyo ameingia kandarasi na klabu ya Arsenal itakayo dumu hadi mwaka 2022.

Klabu hiyo ya Bundesliga imeandika kwenye mtandao wake wa Twitter: “Kila la heri na asante kwa ushirikiano wako kwa muda wote wa miaka sita ya ya kujivuniai.”

Kolasinac aliwasaidia Schalke kumaliza nafasi ya 10 Bundesliga msimu uliopita na kutinga hatua ya robo fainali katika michuano ya Europa League ambapo waliondolewa na klabu ya Ajax iliyotinga hatua ya fainali.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents