Michezo

Arsenal yaongeza matumaini kutinga nne Bora

Arsenal imeimarisha matumaini yao ya kutaka kuwa katika timu nne bora katika msimamo wa ligi kuu nchini Uingereza, kufuatia ushindi wao wa mabao 2-0 dhidi ya Southampton.
Mabao hayo yalifungwa na Alexi Sanchez na Olivier Giroud.

Baada ya kipindi cha kwanza kilichokosa mchezo mzuri, Sanchez aliwashangaza wengi baada ya kuwachenga walinzi wa Southampton na kisha kucheka na wavu.

Giroud ambaye alitokea benchi akichukua nafasi ya Wellbeck aliimarisha ushindi huo kwa kufunga kwa kichwa muda mfupi baada ya kuingia uwanjani.

Southampton hawakufanya mashambulizi mengi katika safu ya ulinzi ya Arsenal.
Fursa yao kuu ilikuwa katika kipindi cha kwanza wakati Manolo Gabbiadini alipopiga mkwaju uliookolewa na Petr Cech.
Ushindi huo unamaanisha kwamba Arsenal inapanda juu ya Manchester United katika nafasi ya 5 ,alama tatu nyuma ya Manchester City.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents