Arsene Wenger aichomolea Fulham dakika za mwisho kabla ya kutangazwa Claudio Ranieri
Aliyekuwa meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amekataa nafasi ya kurithi mikoba ya kocha Slavisa Jokanovic ndani ya klabu ya Fulham inayoshiriki ligi ya kuu Uingereza.
Aliyekuwa kocha wa Arsenal, Arsene Wenger
Kwa mujibu wa Daily Telegraph, mmiliki wa klabu ya Fulham, Shahid Khan wiki iliyopita alizungumza na wagombea wa nafasi ya kuifundisha timu hiyo huku jina la Wenger likipendekezwa kabla ya kumteua Claudio Ranieri.
Kocha wa Fulham, Claudio Ranieri ambaye amechukua nafasi ya Jokanovic
Lakini Mfaransa huyo alikataa na kusisitiza kuwa kamwe hatakuwa tayari kuzifundisha klabu za Uingereza baada ya kuzifundisha kwa takribani miaka 22 akiwa Arsenal na kufanya hivyo ni kuishushia heshima The Gunners.
Fulham kwa sasa inashika mkia kwenye msimamo wa ligi hiyo baada ya kuwa na pointi tano pekee mpaka sasa.
Hii siyo mara ya kwanza kwa Mzee Wenger kuhusishwa kurejea kwenye soka kwani alishawahi kuzungumzwa kutua Real Madrid ambaye kwa sasa imemtangaza Santiago Solari kama kocha mkuu.