Michezo

Arsene Wenger amshauri jambo Gary Neville

Kocha Arsene Wenger ametoa ushauri kwa Gary Neville hii inatokana kufutaia kipigo cha goli 7-0 kutoka kwa Barcelona kwenye mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya kombe la Copa del Rey, Wenger kamtaka Neville kupigania nafasi yake kunako klabu ya Valencia kwa sababu bado hana uzoefu mkubwa hivyo watu kukosa imani naye kama kocha.

Gary-Neville

Beki huyo wa zamani wa Manchester United yupo katika kipindi kigumu, akiwa kama kocha kwa mara yake ya kwanza kabisa kutokana na timu yake (Valencia) kutoshinda hata mchezo mmoja wa La Liga tangu achukue mikoba klabuni hapo.

Wenger amesema Neville anakabiliwa na presha kubwa kutokana na kutokuwa na uzoefu mkubwa na kazi hiyo.

“Mara nyingi huwa naamini kwamba wachezaji wengi wenye majina makubwa huponzwa na majina yao ndiyo maana hupewa timu kubwa mapema na kushindwa kufanya vizuri,” aliwaambia wanahabari.

“Kama sio kocha mwenye jina kubwa basi, ni muhimu kupambana. Hili ni tatizo kubwa kwa sababu mara nyingi huanzi ukiwa juu. Lakini, kwa upande mwingine ndiyo wakati mzuri wa kujifunza.

“Naamini kwamba uzoefu huchukua nafasi kubwa sana kama hujaanza vizuri. Ukiwa na mwanzo mgumu huwezi kuaminiwa kwa sababu hauna historia yoyote ya nyuma inayokubeba, kwamba, pengine ulishafanya mambo makubwa ila ni kipindi cha mpito tu kinatokea.”

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents